Kutunza kumbukumbu za shamba la samaki na masoko

Kumbukumbu ambazo ni muhimu kwa ajili ya kutunzwa ni kama, ukubwa wa bwawa, idadi ya samaki, sehemu mbegu ilipochukuliwa, uzito wa mwanzo wa samaki, tarehe ya kupanda samaki, kiwango cha chakula kwa kila siku/wiki/mwezi, ubora wa maji, mahitaji ya kila siku na gharama zake , tarehe ya kuchukua sampuli, na wastani wa uzito wa samaki kwa kila mwezi.

Umuhimu wa kufahamu vyanzo vya magonjwa ya mifugo

Magonjwa mengi ya mifugo husababishwa na vyanzo kutoka nje ya mwili wa mnyama mfano; mazingira machafu anayoishi mnyama, vitu vinavyopelekea vidonda (vitu vyenye ncha kali) ambavyo husababisha vidonda na baadaye vimelea vinaweza kukaa.

Fahamu ni aina gani ya ng’ombe wa maziwa ni bora zaidi kufuga kwa lengo la kuzalisha

Uzalishaji wa maziwa ni biashara nzuri sana na ya kuvutia ambayo huwa na faida nyingi na humfanya mfugaji kuridhika hasa kwa yule anayependa kazi hii. Hata hivyo, ni lazima kuanza kwa kuweka msingi imara hata kabla ya kufikiria ni aina gani ya mbegu utaichukua kwa ajili ya kufuga. Ni vizuri kufahamu kuwa, usimamizi ni moja ya jambo muhimu sana ambalo likifanyiwa uzembe linaweza hata kumbadilisha ng’ombe wa maziwa kuwa na uzalishaji duni kama ngo’mbe wa kienyeji. Aina mbalimbali za ng’ombe wa maziwa huwa na mahitaji tofauti, hivyo kiwango cha maandalizi yako ni muhimu sana.

Uhifadhi wa malighafi na chakula cha samaki

Usimamizi mzuri na udhibiti wa ubora wa chakula cha samaki ni muhimu sana. Usimamizi na udhibiti wa ubora wa chakula unahusisha mambo muhimu yafuatayo: ufuatiliaji wa karibu wa ubora wa malighafi za kutengenezea chakula (feed ingredients) wakati wa utunzaji, utengenezaji, uchanganyaji na wakati wa kuhifadhi chakula baada ya kutengenezwa.

Unaweza kuongeza pato kwa kuzalisha bamia

Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zao hili hutumika kama mboga inayoliwa matunda. Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limeenea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines. Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za kiasili nazo hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine.

Matumizi

Fahamu ugonjwa hatari wa mahindi MLN

Ugonjwa hatari wa mahindi ujulikanao kwa jina la kitaalamu “Maize Lethal Necrosis Disease” umethibitika kuwepo nchini Tanzania. Ugonjwa huu umeanza kuua matumaini ya wakulima katika harakati za kuendeleza kilimo cha mahindi kama zao kuu la chakula.

Sindika soya ili kuongeza thamani na ubora wake

Soya ni zao mojawapo kwatika mazao ya jamii ya mikunde ambalo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Mtwara,Ruvuma, Morogoro, Rukwa, Lindi,Mbeya, Iringa na Arusha. Zao hili huwa na virutubisho vingi kama vile wanga, protini, mafuta, madini na hata vitamini. Aidha, lina sifa ya kuwa na kiasi kikubwa cha protini kinachofikia hadi asilimia 40.

Njia rahisi za upatikanaji wa vifaranga wengi

Kuna njia tofauti za kuanza au kuongeza mtaji kwa mfugaji wa kuku kama vile, kununua kuku wakubwa, vifaranga kutoka kwa wafugaji wengine au kuzalisha vifaranga wako wewe mwenyewe. Kwa wafugaji wengi ambao wana lengo la kufuga kuku wengi wa umri mmoja na kupata mayai mengi au aweze kuuza kuku wengi kwa wakati mmoja wenye umri unaolingana inabidi uwe na vifaranga wengi wa umri mmoja.

Chanjo huokoa kuku na kuongeza pato

Watu wengi wamekuwa wakianzisha miradi ya ufugaji wa kuku bila kuzingatia kanuni bora za utekelezaji wa mradi huo. Moja ya mambo ambayo wafugaji mara nyingi husahau kuzingatia ni utoaji wa chanjo sahihi na kwa muda muafaka.

Ni muhimu kufahamu mambo unayotakiwa kuzingatia katika kuwapatia kuku chanjo. Wakati wa kutayarisha mpango wa kuchanja kuku kwa ajili ya kinga dhidi ya magonjwa, kuna vipengele vikuu sita ambavyo unatakiwa uvifahamu na kuvizingatia kama ifuatavyo:

Usindikaji wa ndizi umeniwezesha kuanzisha miradi mingine

"Siku zote usipokuwa na juhudi na maarifa maisha ni magumu sana, lakini unapojituma na kutokukata tamaa, ni wazi utapata mafanikio. Jambo la msingi ni kujifunza mambo mbalimbali na kutenda kwa vitendo." Ndivyo alivyoanza kueleza Penina ambae ni msindikaji wa ndizi kutoka kijiji cha Nndatu wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.

Pages