- Kilimo
Sambaza chapisho hili

Tumbukiza ni mbinu inayofaa katika eneo ambalo ni kame na lisilokuwa kame. Ni mbinu ya kuhifadhi maji, na kutoa mavuno mengi zaidi. Ni mbinu ambayo imepokelewa kwa kiasi kikubwa na wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka sehemu ambazo wana eneo dogo kwa ajili ya uzalishaji wa malisho. Ni ufumbuzi ambao umeonekana kuleta ongezeko la uzalishaji wa matete kwa asilimia 20 katika ekari moja. Kama inavyo onekana kwenye picha, mbinu hii inaweza kutumika kwa ajili ya aina mbalimbali za mazao.

Kutengeneza shimo: Lima na usafishe shamba lako vizuri. Chimba shimo lenye upana na urefu wa sentimita 60 kwa 60, au 60 kwa 90, au 90 kwa 90 kulingana na kiwango cha unyevu kwenye eneo ulilopo. Changanya debe 1 la udongo wa juu na debe moja la mbolea (mboji). Weka mchanganyiko huo kwenye shimo ukiacha kiasi cha sentimita moja bila kujaza. Panda mimea/mapandikizi  5-10 kwenye shimo moja.

Kusanya mbolea kwa kutumia shimo

Moja ya changamoto ambazo wakulima wanakabiliana nazo wanapotaka kutumia mbolea mboji, ni kutopata mbolea ya kutosha au yenye ubora unaotakiwa wanapohitaji kwa ajili ya kupandia. Ili kuondokana na tatizo hilo ni kukusanya mbolea. Njia sahihi ya kupata mbolea nzuri ni kwa kurundika kinyesi na mkojo wa ng’ombe pamoja. Njia nzuri ya kuepuka upotevu wa virutubisho kwenye mbolea, inapendekezwa mbolea  kutoka kwenye banda ikusanywe mara mbili kwa siku, kisha kurundikwa kwenye shimo lililotengenezwa maalumu kwa ajili ya kukusanyia mbolea. Hata hivyo ni rahisi kukusanya kwa kuwa wafugaji walio wengi wanafungia ng’ombe kwenye banda lenye sakafu.

Mabua ya mahindi ni mazuri zaidi kwa kukusanya madini (Nitrojeni) kutoka kwenye samadi yanapotumika kama matandiko kwenye zizi la ng’ombe. Wakulima ni lazima wawekeze kwenye shimo la kukusanyia mbolea ili kuhifadhi virutubisho. Ni muhimu pia kupunguza muda wa kuhifadhi; kuongeza matumizi ya mbolea shambani mara kwa mara huongeza rutuba kwenye udongo.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *