- Kilimo
Sambaza chapisho hili

Soko ni mahali au njia ambayo muuzaji na mnunuzi hukutana na kubadilishana mali au huduma. Ni fursa ya kuuaza na kununua.

Kwa kawaida tunapozungumzia soko, tunagusia mambo kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na ukubwa wake, yaani wingi wa wauzaji na wanunuzi katika soko husika, ushindani, washindani, bidhaa na bei zake, changamoto, pamoja na mabadiliko yanayotegemewa.

Kwa upande mwingine, tunaweza kuzungumzia soko katika mgawanyo wa makundi na tafsiri tofauti kama vile:

  • Soko ni mchanganyiko wa shughuli ambazo hufanywa na mjasiriamali katika kuuza mali/mazao  yanayotarajiwa na manunuzi ya wateja/ wadau
  • Ni mchakato wa mategemeo ya matakwa ya wateja/wadau na kutafuta njia ya kuridhishana na kupata faida
  • Ni mahali pa kumleta mteja na kumridhisha kwa faida

Upembuzi yakinifu wa masoko hugusa yafuatayo:

  • Mazao
  • Bei
  • Mahali
  • Na kutangaza bidhaa

Hizi ndizo shabaha za masoko.

Ili kupata soko lenye uhakika na faida kwa wakulima na wafugaji, ni lazima wakahakikishe wanazingatia mambo muhimu yafuatayo.

Mazao

  • Mazao yawe na ubora unaokubalika na soko
  • Yawe na uwezo wa kukaa muda mrefu kabla ya kutumika-Uhai wake ghalani
  • Jina la zao unalozalisha
  • Jinsi ya kufungasha zao hilo (mboga/matunda)katika hali ya ubora na salama.
  • Aina gani ya mbogamboga/matunda unayouza na je, yanaweza kuuzika
  • Mara baada ya kuuza ni huduma zipi zinatarajiwa au kuhitajika.
  • Kuna makubaliano gani unaweza kutoa?

Bei

  • Ni muhimu kufahamu kuwa utauza mazao yako kwa bei gani
  • Je, zao lako litauzwa kwa bei tofauti kwenye masoko mengine?
  • Usambazaji utakuwa mkubwa kiasi gani
  • Utatumia usafiri wa aina gani-baiskeli, pikipiki, gari, kichwa au aina gani?
  • Je, kuna vituo vya usambazaji
  • Jinsi ya kupanga maeneo ya mauzo
  • Ni kiasi gani cha mbogamboga na matunda unaweza kutoa kwa wanunuzi wako
  • Ni wapi utahifadhia mazao yako

Kutangaza bidhaa

Nyanja hii ni muhimu sana kwa biashara yako pia. Hii ni kwa sababu ndiyo inayofanya uweze kufahamika vizuri na bidhaa yako kupata wanunuzi wa kutosha. Fahamu ni njia ipi utatumia kati ya hizi:

  • Kuuza wewe binafsi
  • Kuweka mabango
  • Uhusiano na huduma za kiteknolojia
  • Matangazo kwenye televisheni na redio
  • Mitandao ya kijamii

Ili kufanikisha masomo ni muhimu kufahamu mchanganyiko wa mambo yafuatayo:

  • Wateja wako ni kina nani, wa aina gani, utawafikiaje, njia za usambazaji
  • Mikakati yako ya uuzaji na makisio yake
  • Fahamu washindani wako, waelewe na wasiwe maadui zako
  • Fahamu sehemu za uzito/uwezo wao na madhaifu yao
  • Wanakuzidi nini, na wapi
  • Weka mikakati ya kujaza mapungufu yako

 

Umuhimu wa masoko

 

Wakati uliopita, watu walisema “Tunauza tunachozalisha” usemi huu ni sawa kwa bidhaa fulani ambazo si kila mtu anaweza kuzalisha kama vile saruji.  Siku za leo biashara ndiyo inatafuta wateja wanataka nini kabla ya kuingia kwenye uzalishaji au utoaji wa huduma

 

Wajibu wa muuzaji

 

  • Kutafuta masoko na matakwa yake/mahitaji yake
  • Kusimamia uzalishaji wa mazao, huduma na aina
  • Kuinua bidhaa na huduma
  • Kuchagua na kushawishi njia za usambazaji
  • Kupata mauzo ya mazao na huduma
  • Kupanga makubaliano ya uzalishaji
  • Kupanga na kuratibu shughuli zote za masoko

 

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *