Mbolea ya asili inayotokana na magugu maji

Hii ni aina ya mbolea ya asili isiyokuwa na madhara yoyote kwa binadamu na wanyama. Mbolea hii hutengenezwa kwa kuvundika mimea ya baharini au maotea ya majini. Aina hii ya mbolea inafaa kutumika kwa kuchanganya na viua wadudu vyovyote ambavyo ni asidi au basic kwani utendaji kazi wake hauwezi kupote endapo itachanganywa.

Ugonjwa wa miguu na midomo (FMD)

Huu ni ugonjwa unaowashika ng’ombe, kondoo, mbuzi, pamoja na wanyama wa porini kama mbogo, swala na wakati mwingine tembo. Ng’ombe anapopatwa na ugonjwa wa miguu na midomo huchechemea na asipotibiwa kwa haraka hushindwa kusimama na kula hatimae hudhoofika na hata kufa.

Liki: Zao lisiloshambuliwa na magonjwa

Liki ni moja ya mazao ya mbogamboga ambayo yanapata umaarufu mkubwa nchini Tanzania, kutokana na kuzalishwa katika maeneo mengi, na kuwa na soko la uhakika. Zao hili ni moja kati ya mazao ya mboga ambayo yanaweza kuachwa shambani kwa muda mrefu baada ya kukomaa, ili kusubiri soko endapo kuna tatizo katika soko ikiwa ni pamoja na bei ya kuuzia.

Unaweza kufuga kambale kwenye bwawa

Kambale (Ietalurus Punetaus), ni aiana ya samaki ambao wana majina mengi kulingana na eneo na jamii husika. Samaki hawa unaweza kusikia wakitajwa kwa majina mengine kama vile, kambale channel, koleo, samaki kidevu n.k. Asili ya samaki hawa ni Amerika ya Kaskazini. Samaki hawa hukua kwa haraka sana, na kuwa na uzito mkubwa.

Mwongozo wa ufugaji wa kuku

Ndugu wakulima na wadau wote wa Mkulima Mbunifu, Kwanza Heri ya Mwaka Mpya.

Sasa unaweza kusoma na kupakua kitabu cha Mwongozo wa ufugaji wa kuku' kwenye mtandao kwa kufungua anuani http://issuu.com/mkulimambunifu/docs/mwongozo_wa_ufugaji_wa_kuku_for_web

Dawa ya asili ya kuhifadhi nafaka

Mara nyingi wakulima hupata mavuno mengi katika mazao ya nafaka kama vile mahindi na maharagwe na hulazimika kuhifadhi kwa muda fulani kwa ajili ya kuuza ama kwa ajili ya chakula cha familia zao hasa katika kipindi cha ukame ambapo hakuna mazao yeyote yanayozalishwa. Ili kuyahifadhi mazao hayo kwa muda mrefu na kukinga na wadudu waharibifu, wakulima hao hulazimika kununua dawa ya sumu ya kuhifadhia jambo ambalo si hakika sana kwa afya.

Ni hatari kumfunga mbuzi kamba shingoni

 

Ni dhahiri kuwa wafugaji wengi wana bidii sana na kuwa na matumaini makubwa kutokana na kazi zao. Hari ya kuwa na uzalishaji mzuri kutokana na mifugo yao pia ni dhahiri. Pamoja na hari hiyo, wafugaji wengi wamekuwa hawazingatii kanuni bora za ufugaji na utunzaji wa mifugo yao. Mbuzi wa aina zote wawe wa kisasa au kienyeji wana tabia ya kupenda uhuru na wanahitaji matunzo mazuri ili kuwa na ufanisi mzuri.

Epuka kuchunga mifugo kwenye maeneo hatarishi

Licha ya kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazozalisha mifugo ya aina mbalimbali na kwa wingi kama vile ng’ombe, mbuzi, kondoo lakini inakabiliwa na upungufu mkubwa wa maeneo ya ufugaji sambamba na malisho ya kutosha kwa ajili ya mifugo hiyo. Wafugaji walio wengi, wameshindwa kukabiliana na changamoto hizo hasa kwa kutenga maeneo maalum ya kuchungia au kufuga majumbani, na badala yake wanalazimika kuchunga mifugo hiyo katika maeneo hatarishi na yasiyofaa kwa shughuli hizo.

Magimbi, mkombozi wakati wa njaa

Magimbi ni chakula muhimu chenye kiwango kikubwa cha wanga kinachohitajika katika mwili wa binadamu na moja kati ya mazao makuu ya chakula kama vile viazi mviringo, mihogo na viazi vitamu. Zao hili hulimwa katika sehemu mbalimbali duniani kama barani Afrika, Caribbean, Asia, America na Pacific. Kwa nchi za Afrika, zao hili hutumika zaidi kunapokuwa na uhaba wa chakula, kwani lenyewe hupatikana msimu wote wa mwaka na katika majira yote.

Matumizi

Papai, zao linalozalishwa kwa urahisi

Papai ni tunda lenye ladha nzuri, na rahisi kuliwa. Aina hii ya tunda ni chanzo cha virutubisho muhimu mwilini, ambavyo husaidia kujenga mwili. Zao hili asili yake ni ukanda wa kitropiki ambao hauna baridi kali na joto kiasi.

Udongo

Pages