Zalisha matango uboreshe kipato kwa muda mfupi

Matango (cucumber) ni zao muhimu katika mazao ya mboga na matunda nchini Tanzania na hata nje ya Tanzania. Ni vizuri kuwekea matango fito kwani matunda yake yakilala ardhini huoza. Hili ni zao la biashara, pia chakula. Zao hili hustawi na kulimwa kwa wingi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Pwani.

Kabichi, faida lukuki kiuchumi na kiafya

Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha mimea ya kaulifulawa (cauliflower ), kabichi ya kichina na kale. Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka. Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri.

Mtama silaha ya kukabili uhaba wa chakula

Mtama hutoa mazao mengi hata kwenye hali ambayo haifai kwa kilimo cha aina nyingine za mazao ya nafaka. Mtama una uwezo mkubwa wa kustahimili ukame. Mtama unaweza kutumika kwa kuchemshwa na kuliwa kama ulivyo, kusagwa na kutumika kwa uji, kutengenezea vinywaji kama vile bia, kuoka mikate, na aina nyinginezo za vitafunwa. Mmea wa mtama pia hutumika kwa ajili ya malisho ya mifugo kama vile hay  na sileji.

Jenga nyumba ya nyuki upate faida zaidi

Kufuga nyuki na kuzalisha asali kwa mtindo wa kisasa kwa kujenga nyumba ya nyuki inamwezesha mfugaji kuongeza uzalishaji pamoja na kipato.

Hongera Mkulima Mbunifu

Ni dhahiri kuwa kila mtu anapoanzisha jambo fulani, anategemea kupiga hatua na kupata mafanikio juu ya jambo husika, na kunapokuwa na mafanikio huambatana na furaha isiyo kifani.

VACANCY ANNOUNCEMENT (Ref. No. MKM/AE/01/092013)

Mkulima Mbunifu (MKM) is a Kiswahili magazine that aims to improve access to and utilization of information on sustainable agricultural practices and technologies by small-scale farmers in Tanzania and neighbouring countries. icipe — African Insect Science for Food and Health and Biovision Africa Trust launched a successful pilot project in Tanzania between July 2011 and June 2012 with favourable response from farmers in Arusha, Kilimanjaro, Iringa, and Morogoro areas.

Karanga ni zao muhimu la jamii ya kunde

Karanga ni zao maarufu sana duniani katika kilimo cha mzungunguko. Nchini Tanzania uzalishaji wa karanga ni wa chini sana kutokana na kutokuwa na mvua za uhakika, kiwango kidogo cha teknolojia miongoni mwa wakulima, wadudu na magonjwa, pamoja na kutokuwa na mbegu ya uhakika.

Mipango thabiti huleta mafanikio katika ufugaji

Mipango thabiti huleta mafanikio katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa. Wafugaji waliofanikiwa wanafahamu fika kuwa katika uzalishaji wa maziwa 20% inatokana na aina ya ng’ombe na 80% matunzo. Tumekutana na kupokea maombi kutoka kwa watu wengi ambao wanataka kuanzisha ufugaji wa ng’ombe, lakini hawajui ni wapi pa kuanzia.

Alizeti ni chanzo cha malisho ya mifugo

Alizeti haitoi mailisho pekee, pia inatoa mafuta bora kwa afya ya binadamu na pia malighafi inayotumiwa na nyuki kutengeneza asali. Unapotengeneza chakula cha mifugo peke yako, si tu kupunguza gharama, lakini pia inakupa uhakika wa kuwa na chakula bora. Pia Wafugaji wa nyuki wanaopanda alizeti wanapata faida ya ziada kwa kupata asali iliyo bora kwa sababu nyuki hukusanya poleni kutoka kwenye alizeti wanapofanya ushavushaji.

Pages