Nyanya zinahitaji matunzo ili upate mavuno

Nyanya huzaa vizuri sana hasa zinapowekewa mbolea mboji au samadi iliyooza vizuri. Unaweza kuongeza mbolea ya minjingu kiasi cha kijiko kimoja cha chakula au vijiko 3 vya chai kwa kila shimo. Endapo ardhi ina upungufu wa mbolea asili, inashauriwa kupanda kwanza mimea yenye uwezo wa kutoa mbolea vunde bora kama vile kunde, mucuna, soya au clotalaria kabla ya kusia mbegu za nyanya au kupanda.

Vidokezo juu ya namna ya kulisha kuku

Kuku anayetaga kwa siku huhitaji kiasi cha gramu 130 za chakula pamoja na maji safi wakati wote.

Maji moto (weaver’s ant) wadudu rafiki

Maji moto au Sangara ni aina ya wadudu, ambao ni rafiki kwa mkulima yeyote anayefanya shughuli zake kwa kuzingatia misingi ya kilimo hai. Wadudu hawa huishi katika miti ya mikorosho na miembe. Mara nyingine hupatikana katika pamba. Ikumbukwe kuwa tangu kuumbwa dunia, kila kitu kilikuwa kiasili, watu walikula vyakula na matunda ambayo yalikuwa katika mfumo wa asili bila kuwa na matumizi ya madawa ya viwandani.

Ufugaji wa nguruwe ni rahisi na wenye tija

“Ufugaji wa Nguruwe ni lazima uwe wa kisasa ili kupata mazao bora. Unaweza kupata kila unachohitaji wewe, familia na hata ndugu zako kutokana na ufugaji wa nguruwe”, anasema Bwana Lomaiyani Molel kutoka Arusha. Jamii nyingi hapa Tanzania huchukulia nguruwe kama mnyama mchafu na asiyefaa kuwa karibu naye na hata kwa matumizi kama lishe. Zaidi, nyama yake inapendwa na haina madhara kwa afya na inapendekezwa kuliwa zaidi kuliko nyama nyekundu.

Soya zao lenye manufaa lukuki kwa jamii

Maharagwe ya soya ni moja ya mazao muhimu katika jamii ya mikunde katika nyanja za uzalishaji wa kibiashara kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha protini (35-40%). Soya inatumika katika kuandaa vyakula vinavyoliwa vikiwa vibichi, vinavyovundikwa na vyakula nikavu, mfano maziwa, tofu, mchuzi pamoja na kimea.

Hali ya hewa, udongo na maji

Ufugaji wa nyuki ni kazi nzuri ya ziada

Ufugaji wa nyuki unaweza kuwa chanzo kizuri cha kipato cha ziada kwa wakulima wadogo wadogo. Uzalishaji wa asali nchini Tanzania umekuwa ukitegemea sana wafugaji wadogo wadogo, wanaotumia njia za kiasili kama vile mizinga ya magogo au vyungu, kwa nyuki wa kiafrika ambao ni wengi sana kwenye mapori.

Hatua sita za kupata udongo bora shambani

Ili kuwa na kilimo chenye mafanikio mkulima anatakiwa kufuata hatua sita za kuboresha udongo.

1. Usiuchoshe sana udongo

Mahitaji ya ng’ombe ili aongeze maziwa

Wape ng’ombe wako lishe kamili, yenye nguvu, protini, na vitamin pamoja na maji ya kutosha. Kulisha ng’ombe kwa kutumia aina yoyote ya malisho haitoshi kukuhakikishia ng’ombe anakuwa na afya nzuri na kutoa maziwa ya kutosha. Kama ilivyo kwa binadamu, ng’ombe anahitaji mlo kamili. Malisho ni lazima yawe na uwiano sahihi wa viungo.

Njia rahisi ya kutengeneza mbolea maji

Mkulima anaweza kupunguza gharama, kuongeza rutuba kwenye udongo, mavuno pamoja na kipato kwa kutengeneza mbolea mwenyewe. Mimea inaweza kukuonyesha inahitaji nini. Ni rahisi sana kugundua endapo mimea haipati virutubisho vya kutosha. Majani kubadili rangi ni ishara tosha kuwa mimea ina upungufu wa virutubisho. Ni lazima mkulima awe tayari kutatua tatizo hilo kwa haraka kabla hali haijawa mbaya.

Jinsi ya kuzuia magonjwa ya kuku

Ufugaji wa kuku una faida kubwa, lakini mkulima anatakiwa kuzuia kadri awezavyo uwezekano wa kuwepo magonjwa shambulizi.

Pages