Jinsi ya kuzuia magonjwa ya kuku
July 28th, 2011
<< rudi


Ufugaji wa kuku una faida kubwa, lakini mkulima anatakiwa kuzuia kadri awezavyo uwezekano wa kuwepo magonjwa shambulizi.


Wafugaji wengi wamekuwa wakiwekeza katika ufugaji wa kuku. Ufugaji huo unalenga kuku wa kisasa au wa kienyeji. Wanajenga mabanda, kununua chakula, pamoja na kuku, wakitarajia kupata faida kubwa kutokana na uwekezaji huo. Hata hivyo, mradi unapoanza mambo huonekana kwenda sawa, mpaka mfugaji anaposhtuliwa na mlipuko wa magonjwa ambayo hupunguza uzalishaji au kuua kuku.


Mfugaji anaweza kufanya nini kupunguza hatari hii?

Mbinu zinazotumiwa na wakulima duniani kote zinanaonesha kuwa kuweka banda katika hali ya usafi, kuwalisha kuku ipasavyo na kuwapatia maji safi, ndiyo njia ya kwanza muhimu ya kupambana na magonjwa, kama vile mharo mwekundu, kipindupindu cha kuku, na ndui. Kuwa makini katika ufugaji wa kuku ni pamoja na kutoa chanjo kwa kuku, kuzuia magonjwa kama sotoka au ndigana na ndui.


Taratibu za kufuata ili kuzuia magonjwa


Utunzaji wa banda la kuku
• Ni lazima nyumba ya kuku iwe safi na kavu muda wote

• Nyumba ya kuku iwe na nafasi za kupitisha hewa ya kutosha ili kuepuka joto na unyevunyevu

• Hakikisha unaondoa matandazo na takataka zote kwenye banda wakati wote. Matandazo na taka zinaweza kuwa mbolea nzuri ya mboji kwa mimea yako.

• Fagia banda na kuhakikisha ni safi wakati wote. Weka matandazo mapya mara kwa mara.

• Weka nafasi ya kutosha kuku kupumzikia, viota vya kutosha, na kuweka maji sehemu ambayo ni rahisi kusafisha.

• Hakikisha unaondoa wanyama kama panya na wadudu nyemelezi kwenye sehemu ya malisho ya kuku kwani wao hubeba vimelea vya magonjwa.



Utunzaji wa kuku
• Toa chanjo muhimu kwa kuku ili kuzuia magonjwa kama utakavyoshauriwa na mtaalamu wa mifugo. Chanjo huanza katika wiki ya kwanza (mfano chanjo ya kuzuia sotoka) na inaweza kurudiwa baadaye.

• Epuka kuweka kuku wengi mahali pamoja kwani ni rahisi magonjwa kuenea kwa haraka kuku wanaporundikana.

• Tenganisha vifaranga na kuku wakubwa (isipokuwa kutoka kwa mama) kwa sababu vifaranga ni rahisi na wepesi sana kushambuliwa na magonjwa.

• Weka mipaka na madaraja ya sehemu za kuku kuzunguka/kucheza.


Ulishaji

• Wapatie kuku chakula cha kutosha na chenye virutubisho vyote. Unaweza kuwaongezea majani, makombo, nafaka, mchanga laini, au maganda ya mayai.

• Wapatie kuku maji safi muda wote. Wafugaji wengi wameripoti kuwa na matokeo mazuri baada ya kuchanganya dawa ya kuua vimelea kwenye maji ya kunywa.

• Safisha vyombo vya kulishia na kunyweshea kila siku. Osha, sugua vizuri, kisha suuza kuondoa utando unaobeba bakteria.

• Nunua chakula kwa wauzaji wazuri na wanaoaminika ili kuepuka minyoo na sumu hatarishi.

• Hifadhi chakula cha kuku katika sehemu kavu isiyo na joto na isiwe kwa zaidi ya miezi mitatu ili kuepuka kuharibiwa na fangasi.

• Usiwape kuku chakula chochote kinachoonekana kuoza au kunuka uvundo. Kukabiliana na magonjwa

• Muone mtaalamu wa mifugo mara uonapo dalili zozote za kuumwa kwa mifugo wako.

• Watenge na uwapatie tiba au kuwaua na kuteketeza kabisa kuku wagonjwa kuepuka kuenea kwa magonjwa.

• Ondoa ndege waliokufa mara moja, uwafukie au kuchoma moto. Usile kuku aliyekufa. Baadhi ya magonjwa ya ndege yanaweza kuambukizwa kwa binadamu.

• Endapo kuna mlipuko wa ugonjwa katika eneo lako, usiruhusu watu kutembelea banda lako. Watu wanaweza kuleta maambukizi kwa miguu yao katika mabuti, nguo na mikono. Pia magari yanaweza kuleta madhara kwa mabanda yako kupitia matairi na upakuaji wa mizigo.


Ukaguzi wa mara kwa mara

Kila siku

• Safisha vyombo vya kulishia na kunyweshea pamoja na viota.

• Ondoa kinyesi.

• Waangalie kuku wako kwa makini ili kujua afya na maendeleo yao.


Kwa wiki
• Ondoa matandazo machafu na kuweka mapya.


Kwa mwezi
• Angalia uwepo wa wadudu na chawa, kisha utibu kama kuna ulazima.


Zingatia haya kabla ya kuleta mifugo wapya bandani

1. Ondoa matandazo yote, vyombo vya kulishia na kunyweshea.

2. Ondoa uchafu wote unaoonekana bandani.

3. Safisha banda lote kwa kutumia maji na dawa.

4. Suuza na uache likauke.

5. Puliza dawa ya kuua wadudu.

6. Weka matandazo mapya, weka viombo vya kulishia na kunyweshea.

Itikio 37 kwa “Jinsi ya kuzuia magonjwa ya kuku”

  1. friberg ayo anasema:

    nimesoma ndo naanza kufuga naomba ushauri wenu zaidi

  2. Elias anasema:

    Nashukuru kupata na kuona tarifa zenu na nimependezwa zaidi na ufugaji wa kuku,Nataka kuanza na nipo kwenye maandalizi na nilipata taarifa au habari juu ya chanjo mpya ya kuku iliyozinduliwa na chuo cha kilimocha Morogoro Sua je mna taarifa yoyote juu ya chanjo hiyo?

  3. Benson anasema:

    kama unao kuku white leghon naomba tuwasiliane 0713 236223 kwa yeyote yule mie ninao Redhe island red na kuchi chotara

  4. BENSON anasema:

    kama unao kuku white leghon naomba tuwasiliane 0713 236223 kwa yeyote yule mie ninao Rhode island red na kuchi chotara
    pia tunaangua vifaranga na kuuza,mashine za kuangulia incubator zinapatikana pia

  5. 0784608074 anasema:

    Ninao Kuku Weupe Ila wanaumwa. Ugonjwa wamevimba macho yana mavitu kama majipu makubwa wanakuwa vipofu hawali yaani sielewi kabisa walikuwa 200 wamekufaaaaa wamebaki kama 15-20 kwa kweli imenichnaganya sana naombeni msaada wenu 0784608074

  6. Athumani anasema:

    Nahitaji vifaranga vya Rhode Island Red Chicken kwa yeyote anaejua vinapopatikana anielekeze.

  7. stelaah ifunya anasema:

    mnapatikana wapi ninataka mafunzo ya kufuga kuku

  8. AKYOO ELIUD anasema:

    Hakika jarida lenu ni zuri sana, leo ndiyo mara yagu ya kwanza kulina ktk mtandao, ushauri wangu fanyeni hima liwafikie wakulima wadogo ambao ndio wahitaji wakuu na wengi wao wapo vijijini.

  9. malimi mabondo anasema:

    Nahitaji mbegu nzuri za kuku wa kienyeji, nitapataje? na ushauri zaidi kwani bado najifunza ufugaji bora.

  10. John anasema:

    Naomba unitumie design nzuri ya banda la kuku lenye uwezo wa kuchukua kuku 500. Nashindwa namna ya kudesign ikiwa nia pamoja na sehemu muhimu za kutagia hao kuku.

  11. Mwakalobo anasema:

    Nashukuru kwa aliyefanya utafiti na kuandika makala haya ya jinsi ya kuzuia magonjwa ya kuku. Mimi natamani kufuga kuku hasa wa kienyeji lakini kila idadi ya kuku inapoongezeka mara hushambuliwa na magonjwa ya mlipuko sasa nina kuku kama 30 tu, wengi wamekufa kwa ugonjwa wa jicho kuvimba na wengine kutoa choo cha rangi ya kijani na wengine wanasinzia na kukosa hamu ya kula naomba nisaidieni nitumie dawa gani? ebu naomba elezea angalau kila ugonjwa wa kuku na tiba yake, itusaidie tulioko mbali na mijini. ahsante.

  12. Priscilla anasema:

    somo zuri nimelipenda, naomba unifahamishe wapi nitapata vifaranga wa kienyeji nianze ufugaji?

  13. Felix Sanga anasema:

    Asanteni sana kwa mafunzo mnayotupatia
    Kwa kawaida mtu anayeanza kufuga anatakiwa awe na mtaji kiasi gani?
    Halafu wastani wa bei ya kifaranga kimoja ni shiling ngapi?

  14. Oliveirn Mwamalili anasema:

    Mimi ni mtaalam wa Mifugo na Kilimo unaweza kunitafuta kwa namba 0653222356 na 0756222356 kwa kusaidiana kutibu magonjwa ya mifugo na Mimea au Mazao mbalimbali.

  15. Issa Mahamba anasema:

    Nahitaji kufuga kuku wa kienyeji nao kujua magonjwa ya kuku na dawa za kutibu na kinga.

  16. Baba H anasema:

    Naombeni mwenye design nzuri ya Banda la kuku kama 500 anitumie picha plz, pia kama unao aina nzuri ya kuku naomba mnipatie mbegu.

  17. Francis Kazoba anasema:

    Safi sana hii, ni lengo langu kufuga, kwa kuanza naomba design ya banda la kuku. baada ya hapo nitapenda kujifunza kwa kuwatembelea wafugaji waliobobea

  18. Juliana anasema:

    Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji, shida yangu kubwa ni kuomba ushauri wenu kwani kuku wangu wanagonoana sana. Nitumie njia gani kuzuia hali hii. Pia nawapongeza sana waliokubali kuweka wazi mawazo yao kwenye tuvuti hii. Hongereni sana na mbarikiwe na bwana kwa kuokoa wafugaji wadogo wadogo kama mimi. Nimefurahishwa na comments zenu.

  19. Arthur Temba anasema:

    Nimevutiwa sana na ukurasa huu. Umenifungua vitu vingi. Mimi ni mfugaji mdogo wa kuku wa mayai. Ninaomba mtuwekee kalenda ya chanjo kwa magonjwa mbalimbali tangu tunapopokea vifaranga hadi wanapokuwa wakubwa.
    Pia nauliza, wapi nitapata vifaranga weupe wa mayai. Ahsante

  20. Revocatus Mgawe anasema:

    Nimefurahishwa sana na mawazo ya wote waliochangia na pia niwapongeze wataalam wote ambao wameelimisha.
    Ninapenda kuuliza je naweza kupata wapi incubetor yenye uwezo wa kuchukua mayai kuanzia 1000.

  21. Willy stanley anasema:

    Mie ni mwanza ni wapi? Naweza pata majogoo wazuri wa rhode island red, black australop na white leghorn naomba tuwasiliane kwa namba hii 0752808500 nitashukulu sana kama mtanipa ushirikiano chanya asanteni mungu awa bariki

  22. mary anasema:

    Nimesoma jarida lenu japo nimechelewa lakini naamini nimefaidika. Mimi ninatafuta kuku wa cox wazuri. Mara ya kwanza nilichukua 600 mkuza wakafa wakabaki 30 sasa sijajua nichukue kampuni gani zaidi.

  23. Mwang'oko Milamo anasema:

    Juliana wape dagaa na majani ama mboga mboga kwa wingi itakua mbadara wa kudonoana. je ulikua unatumia damu ya mifugo katika mchanganyiko wa chakula na umeacha?

  24. Mwang'oko Milamo anasema:

    Mary nmaomba ufanye utafiti ni kwanini hao wa kwanza walikufa kabla huja tafuta kampuni nyingine

  25. Jones Mbalilaki anasema:

    0754438822/0786438822

  26. Anna A. Nsuri anasema:

    Ndugu Mwakalobo si lazima uwe kwenye miji mikubwa ndipo upate ushauri wa kitaalam. Hata katika eneo uliko huduma za kitaalam zinapatikana. Waone wataalam wa mifugo watakuelimisha. Hata hivyo kuku wako wanahitaji lishe bora, chanjo mbalimbali kama vile chanjo ya ndui, kideri gumboro na dawa ya minyoo. Usafi wa banda na wa vyombo vya chakula ni wa muhimu sana katika kuzuia magonjwa ya kuku. Tuendelee kuwasiliana kwa material zaidi.

  27. Monica Kimario anasema:

    Mwakalobo Nakushauri usichanganye kuku wageni unaowanunua na pia uwe unatenga kuku wagonjwa mapema kabla hawajaambukizana. Jitahidi pia kuwapa antibiotic kama ESB3. Hata hivyo tuwasiliane kwa ushauri zaidi.

  28. saidi emanuel anasema:

    mimi napendekeza katika majarida yenu mtenganishe kilimo na mifug kama ilivyo sasa katika vyuo(chapisho la kilimo pekee, hivyo pia mifugo)kufanya hivyo utasababisha mlengwa kusoma kinachomhusu akaelewa saidi emanuel labarani mwanachuo cha kilimo niko likizo bukoba

  29. Issa mahamba anasema:

    Nimeanza kufuga kuku na sasa namiliki kuku 900 wakubwa wadogo huenda wakafika 600 natafuta dawa za kienyeji za magonjwa mbalimbali.

  30. ISSA SAWE anasema:

    Naomba kujua namna ya kutengeneza brooder kwa ajili ya kukuzia vifaranga. mawasilino yangu 0756773697

  31. Francis Kulwa anasema:

    hongereni sana kwa somo zuri.. mimi nipo tabora nahitaji mashine ya kuangulia vifaranga ya kutumia mafuta ya taa kwani huku ninakoishi hakuna umeme. mawasiliano ni fkulwa@rocketmail.com

  32. Mwang'oko Milamo anasema:

    issa tumia alovera hii nime tumia kwa kuku wa kienyeji na jamii ya malawi, inasaidia ponda ponda na weka kwenye maji kama una weza hata kila siku sono mbaya, na majani ya mpapai hii nimesomatu ila bado sijaanza kutumia

  33. Sara anasema:

    Habari, naomba ushaur kuku wangu wa mayai wanasumbuliwa na mafua niwape dawa gani?

  34. Didas kaika anasema:

    Ni kweli ufugaji wa kuku unamsaidia mkulima.nashauli mfugaji anayeanza ufungaki wa kuku aanza na kuku wachache.iliaweze kuwaelewa zaidi tabia,magomjwa pamoja na tiba zake.wapo watu au mtu akisikia kuku zinalipa anaagiza vifaranga matokeo yake nikishindwa kifuga na kuwauza kabla yakutaga.pata ushauli zaidi kabla yakufuga.0762837909 Tarime

  35. kasunga anasema:

    nashukulu kwa elimu yenu

  36. Magreth anasema:

    Nashukuruni sana kwa mada nzuri mimi ndio kwanza nimeanza rasmi kufuga kuku wa kienyeji mwez huu ila nimeanza na vifaranga leo ni siku ya 10 ila karibu vyote vinasinzia inafika mahali nakata tamaa kweli cjajua tatizo ni nini na wala sijui dr wa mifugo niko dar naombeni ushauri wenu namna ya kufanya.

  37. Mwang'oko Milamo anasema:

    Dada Magreth usichoke. rudisehemu ulionunua watakusaida au nipigie 0753390755, 0718799395 tujadiiane

Weka majibu yako hapa