Viota bora ni muhimu kwa ajili ya kuku

Kuku anapotagia porini, mayai huliwa na wanyama kama vile nyoka na wengineo. Kuku pia anaweza kudhuriwa na wanyama hao na wakati mwingine kuibwa. Viota ni mahali ambapo kuku hutaga mayai, kuhatamia na kuangua vifaranga. Hii inamaanisha kuwa viota ni sehemu muhimu sana ya kuzingatia ili kuweza kupata mayai mengi yaliyo salama pamoja na vifaranga.

Aina za viota

Kuna makundi mawili ya viota vinavyotumiwa na kuku pamoja na ndege wengine wafugwao.

Kiota kilicho tengenezwa na kuku mwenyewe

Hii ni aina ya viota ambavyo kuku huchagua mahali pa kutaga na kuhifadhi mayai. Inaweza kuwa mahali popote ambapo kuku ataona mayai hayataweza kudhurika au kuonekana. Kwa mfano, vichakani, stoo au kona yenye giza. Njia hii si nzuri kwani husababisha upotevu wa kuku na uharibifu wa mayai.

Kwa kutagia stoo au sehemu iliyojificha ya ndani, japokua ni sehemu salama ambayo haiwezi kufikiwa kirahisi na wezi au wanyama, mayai yanaweza kuharibika. Kuku akitaga sakafuni, sehemu yenye nailoni au magunia mayai yanaweza kuharibiwa na unyevu. Mayai hayo si mazuri kwa kutotoleshea. Itabidi mfugaji ayatumie au ayauze kwa ajili ya chakula.

Katika ufugaji wa ndani, kuku hutaga mayai sehemu yoyote hasa kipindi ambacho kuku huanza kutaga. Hii husababisha mfugaji kuyakanyaga mayai kwa bahati mbaya au kuku wenyewe kula mayai hayo na kupunguza uzalishaji wa mayai.

Kiota kilicho andaliwa na mfugaji

Kuku wanapotengenezewe viota vizuri huhatamia kwa utulivu kuongeza uzalishaji

Hii ni aina ya viota vilivyo andaliwa kiustadi na kuwekwa mahali stahiki kwa kumrahisishia kuku sehemu ya kutagia. Viota hivi huwekwa ndani ya banda au sehemu nyingine iliyoandaliwa. Viota vya aina hii huandaliwa kwa kuzingatia idadi ya kuku wanaotarajiwa kutaga, pamoja na upatikanaji wa vifaa vya kutengeneza viota.

Mahitaji

Unaweza kutumia vifaa kama vile boksi la karatasi, mbao, nyasi, nguo aina ya pamba (isiwe ya tetroni), matofari na maranda. Boksi, tofali, na mbao husaidia kutengeneza umbo na ukubwa wa kiota. Nyasi maranda na nguo (viwe vikavu) husaidia katika uhifadhi wa mayai yasiharibiwe na unyevu, pia ni mazuri kipindi cha kuhatamia kwani hutunza joto.

Ukubwa wa kiota unatakiwa uwe ni wa kumwezesha kuku kuenea na kujigeuza. Hii ina maana kuwa unatakiwa uwe wastani wa sentimita 35 upana sentimita 35 na urefu sentimita 35.

Namna ya kupanga viota kwenye banda

Ili kuwa na ufanisi mzuri, inabidi idadi ya viota kwenye banda iwe robo tatu ya matetea yaliyofikia umri wa kutaga. Hii huondoa msongamano wa kutaga katika kiota kimoja. Kwa mfugaji mwenye kuku wengi inampasa kuchagua vifaa ambavyo atajengea viota vinavyoweza kutumia eneo dogo na huku akipata viota vingi.

Kwa kuku wanaohatamia, inabidi watengewe chumba chao ili kuzuia uchanganyaji wa mayai. Kila sehemu katika banda si nzuri kuweka viota. Hivyo, katika uchaguzi inakupasa uzingatie mambo yafuatayo:

• Viota visiwe karibu au chini ya kichanja cha kupumzikia, vyombo vya chakula na maji.

• Kiota kisiwe sehemu ambayo mfugaji atakua anapitapita. Mfano, karibu na mlango au dirisha.

• Kiota kisiwe mkabala na sehemu ambayo upepo mkali au mwanga utakua unaingia.

Wakati wa ujenzi wa banda unaweza kujenga vyumba viwili ambavyo kimoja kikubwa utatenga sehemu ya chakula, maji na sehemu ya kupumnzika.

Chumba cha pili utatengeneza viota tu ili kuku anayetaka kutaga aende huko. Kwa kufanya hivyo, kuku wachache watakua wakienda chumba hicho, na usumbufu kwa kuku wanaotaga utakuwa mdogo.

Kulingana na kiasi cha nafasi, unaweza kujenga viota mwisho wa banda na vyombo vya chakula na maji upande wa mbele karibu na mlango. Hii itasaidia kuku kushinda sehemu yenye chakula na maji hivyo kuepusha usumbufu kwenye viota.

Kuku wanaohatamia

Viota vya kuku wanaohatamia inabidi viwe sehemu tofauti na viota ambavyo kuku wanatagia mayai kila siku. Hii itasaidia kuzuia uchanganyaji wa mayai yaliyoanza kuhatamiwa na mapya. Viota hivyo viandaliwe vizuri kwani hukaa na mayai kwa muda mrefu. Ni vema kuwatenga kuku katika chumba chao ambapo watapatiwa maji na chakula.

Umuhimu wa viota

• Kwa kuwa na viota vya kutosha itapunguza usumbufu wa kuingia kukusanya mayai kwa mfugaji.

• Njia mojawapo ya kuzuia kuku kula mayai.

• Upotevu wa kuku na mayai utapungua.

• Utapata mayai bora kwa ajili ya kutotolesha.

• Kupunguza mayai kupasuka, pia mayai kuwa safi.

• Kuku kuwa huru wakati wa kutaga au kuhatamia.

   

Maoni

Viota ni muhimu sana, Ila niliwahi kutembelea Kenya kwa wafugaji wa Kenya, kwa kweli nilifurahishwa na jinsi wanavyo jenga viota vyao, Yaani unaweza ukawa unaokota mayai bila kuingia ndani ya Banda ni njia znuri sana.

mimi nataka kuanza kufuga kuku wa kienyeji, nataka nianze na kuku 20 sasa naomba muongozo wenu ili nipate mazao bora kwa sasa na kwa baadae na kama kuna soft copy yoyote ya instruction plz naomba mnipatie [email protected]

ndugu wafugaji hongereni na majukumu,molinda poultry farm pamoja chasha poultry farm wanao vifaranga wa aina mbalimbali kama vile kroiler,kari,kenbro,na,new southern hemishire,vile vile tunauza mashine za kuangulia vifaranga za kuanzia mayai mia tano na zaidi machine zote no automatic bei ni nzuri sana

kuhusu mashine za kuangulia vifaranga na vifaranga wasiliana nasi kwa simu namba
0767 69 10 71 chasha poultry farm
wax ml
0754 91 70 85 molinda poultry farm

Nimeanza kufuga kuku wakienyeji mwezi huu naomba munipe kanuni ya kutengeneza. chakula cha vifaranga hadi kukua na kuku wa kutaga

Nawashukuru sana kwa kutoa Elimu ya Ujasiliamali kwa ujumla hasa kwa swala la kilimo kwa ujumla yaani kilimo na ufugaji.
na mambo yanayomkomboa mkulima hasa sisi wa hali duni vijijini. Elimu yenu ni nzuri sana na inaleta mabadiliko hasa pale tu mtu anapoipata na kuifanyia kazi vilivyo.
Nawaomba kutumiwa hard copy au vitabu kwa anuani:EZEKIEL NYANGINYWA S.L.P 981, NJOMBE-TANZANIA. SIMU:0763448335
vijijini mtandao huwa sio mzuri kama mjini; kule hakuna 3g wala TTCL ambayo hurahisisha spidi ya mtandao katika usomaji na ufunguaji wa mtandao. tena hata umeme ni shida sana hasa mashambani. Natanguliza shukrani zangu kwa kukubaliwa na kutumiwa Vitabu na vipeperushi mbalimbali. Asanteni na mungu awabariki sana.

Nashukuru sana kwa taarifa na ombi lako ni zuri. Ili kuweza kutumiwa vijarida vyetu, mnatakiwa muwe katika kikundi cha watu kuanzia watano na kuendelea,kama uko mwenyewe tutakuomba tafadhali uendelee kusoma kwenye tovuti wetu.

Ukishakuwa kwenye kikundi, tutumia jina la kikundi, sanduku la posta, jina la mwenyekiti na nambari yake ya simu

Naitwa ABEL SENG’ONGO.Nauza na kusambaza AUTOMATIC COMPUTERIZED INCUBATOR za Kisasa Kutoka JAPANI na zenye uwezo wa kutumia SOLA,GENERATOR na UMEME,Kuanzia mayai 60,100,170,500,1000,2000,4000,6000,8000 hadi 10,000 au kulingana na mahitaji yako.ZINATUMIA SYSTEM YA KOMPYUTA KUGEUZA MAYAI,KUONGEZA NA KUPUNGUZA JOTO,KUONGEZA NA KUPUNGUZA UNYEVUNYEVU,INACONTROL OKSIJENI INAYOTAKIWA.
:MAYAI :BEI
Mayai-528— bei-2,000,000/=
Mayai-1056—bei- 3,500,000/=
Mayai-8448 –bei-12,000,000/=
mayai-48—- bei-400,000/=
Mayai-96—bei- 500,000/=
MASHINE YA KUNYONYOLEA KUKU MMOJA KWA SEKUNDE 10 NI 1,500,000/=
WASILIANA NAMI KWA 0765313355 au 0788384285 au 0653557474 E-mail [email protected]
UTALETEWA MPAKA MLANGONI

Asante kwa taarifa

Nimevipenda sana hivi viota

Karibu sana

Kuku kukua ni mradi wa ufugaji wa kuku wa asili kibiasra. .tunakipesha
vifarang. Si mu 0718503330. Tajirika na kuku kukua

Nashukuru sana ABEL.MUNGU akubariki sana,Incubator yangu imefika salama mpaka mlangoni kama ulivyoniahidi na tayari imeshaanza kazi.Sijawahi kuona mashine kama hii.Naomba uendelee kuwakomboa wote waliokuwa wanateswa na mashine za mitaani kama mimi

Asante sana kaka yangu Abel kweli wewe ni muaminifu sana.Tunalisubiri sana hilo Roli letu hapa mbeya kwa hamu yani furaha mpaka usingizi hauji

Asante sana kaka yangu Abel kweli wewe ni muaminifu sana.Tunalisubiri sana hilo Roli letu hapa mbeya kwa hamu yani furaha mpaka usingizi hauji.Asante Abel

Dah!yan ABELI hapa Arusha tumejumuika wote tunaolisubiri loli letu la Incurbator kwa hamu kali sanaaaa.Tunavunja mbavu za mbuzi na vinywaji murua tukilisubiri loli letu.yani ni furaha ilioje laiti ungejuwepo hapa ni furaha kwenda mbele.Tunashukuru sana kwa wema wako.

Tunawashikuru kwa kuelimishana na kusaidiana, karibuni Mkulima Mbunifu

pole kwa kazi, mimi ni mfungaji wa wilaya ya kilombero, ninakumbana na magonjwa ya kuku sana naomba maelekezo zaidi toka kwenu

Habari,

Ni vyema tukajua ni aina gani ya ugonjwa unaokumbana nao au hata dalili zake.

Pia katika tovuti yetu www.mkulimambunifu.org soma nakala ya jarida la mkulima mbunifu toleo la 25 Oktoba, 2014 ukurasa wa 4 na 5, na toleo la 26 Novemba, 2014 ukurasa wa 4 na 5. Hapo kuna baadhi ya magonjwa yanayowakumba kuku tumeyaeleza na namna ya kukabiliana nayo.

Je unataka kufuga kuku wa kienyeji na kutajirika haraka? Wasiliana nasi. Tunatoa mikopo ya kufuga kuku wa kienyeji. Kila kitu kuanzia Vifaranga, madawa, chanjo, chakula na vyombo vyote. Tuna kuunganisha an soko pia. KUKU KUKUA, 0766503330 AU 0718503330. Kwa wanaoishi mikoa ya Dar es salaam, Kilimanjaro, Arusha na Mwanza. KUKU KUKUA; PAMOJA TUPUNGUZE UMASIKINI.

Napenda kuuliza kuhusu ufugaji bora wa Bara wa kawaida na hasa kuhusu utotoaji na pia soko lake

Habari,
Niko kwenye ujenzi wa banda la kufugia kuku Wa kienyeji.Nimevutiwa na suala mikopo hasa vifaranga, vyombo, madawa na namna ya urejeshaji wa mkopo. Nijulisheni bei kwa kila kifaranga na vyombo. Pia nijulishe kama mnautaratibu wa kusafirisha. Niko kasulu-kigoma. Waweza pia kunitumia ujumbe mfupi kupitia 0766257010.

Habari,

Sisi kama mkulima mbunifu hatujihusishi na mikopo wala usambazaji wa vifaranga au vifaa vyovyote vya ufugaji zaidi ya kutoa elimu kwa njia ya majarida na kupitia tovuti yetu hii. Taarifa za mikopo huenda ikawa zinawekwa na watu binafsi wanaojishughulisha na kazi hizo lakini si taasisi ya Mkulima Mbunifu.

Andika maoni mpya

Plain text

  • Hakuna vishikizo vya HTML vinavyokubaliwa
  • Anuani ya ukurasa kwenye mtandano na anwani za barua pepe hubadilika kuwa viungo moja kwa moja.
  • Mistari na aya zinajipanga zenyewe.