Njia rahisi za upatikanaji wa vifaranga wengi

Kuna njia tofauti za kuanza au kuongeza mtaji kwa mfugaji wa kuku kama vile, kununua kuku wakubwa, vifaranga kutoka kwa wafugaji wengine au kuzalisha vifaranga wako wewe mwenyewe. Kwa wafugaji wengi ambao wana lengo la kufuga kuku wengi wa umri mmoja na kupata mayai mengi au aweze kuuza kuku wengi kwa wakati mmoja wenye umri unaolingana inabidi uwe na vifaranga wengi wa umri mmoja.

Kwa nini kuwa na vifaranga wengi wa umri mmoja?

Kupunguza gharama za ufugaji kwa mfano chanjo na tiba;

 • Kutunza kuku kitaalam kwa urahisi
 • Kupata mayai mengi kwa wakati mmoja
 • Kuuza kuku wengi kwa waakti mmoja
 • Kuwapa uhakika wateja wako

Hivyo kuna njia kuu mbili za upatikanaji wa vifaranga wengi kwa wakati mmoja nazo ni;

 1. Kwa kuhatamiza kuku wengi kwa wakati mmoja
 2. Kwa njia ya mashine ya kuangulia incubator)
 3. Njia zote mbili huweza kutoa vifaranga bora bali uchaguzi wa njia ipi itumike utatokana na mtaji wa mfugaji na mahali alipo.

Kwa kuhatamiza kuku wenyewe

Njia hii hutumika kuhatamisha tetea wengi kwa wakati mmoja hivyo mfugaji anatakiwa achague mitetea, mayai, aandae viota, maji na chakula bora.

Sifa za tetea wa kuhatamia

 • Kuku mwenye umbo kubwa
 • Mwenye uwezo na historia nzuri ya kuhatamia na hatimaye kutotoa vifaranga

Sifa za mayai ya kuhatamisha

 • Mayai ya siku ya mwisho kutagwa ndio yawe ya kwanza kuwekwa yafuatiwe na ya siku zinazofuata yasizidi wiki mbili tangu kutagwa
 • Lisiwe kubwa sana au la duara, lisiwe na uvimbe
 • Yasiwe machafu wala yasiwe na nyufa

Sifa za kiota na chumba cha kuhatamia

 • Kuku wanaohatamia watengwe katika chumba ili kuondoa tatizo la kutagiana.
 • Mlango na dirisha viwekwe wavu ili muda wa mchana mwanga na hewa uweze kuingia ndani.
 • Chumba kiwe na nafasi ya kutosha kuweka viota, chakula na maji.
 • Ili kutumia eneo vizuri viota vinaweza kutengenezwa ukutani kama mashelfu.
 • Viota viundwe vizuri kwa nyasi, maranda makavu ya mbao, au nguo ya pamba lakini isiyo tetroni.
 • Viota visiwe sehemu yenye unyevunyevu.
 • Idadi ya viota vilingane na idadi ya matetea walio chaguliwa kuatamia
 • Vinyunyiziwe dawa ya kuuwa wadudu kama utitiri kwani hawa ni wadudu wasumbufu ambao husababaisha kuku kutokatoka nje, hivyo kupunguza uwezekano wa mayai kuanguliwa yote.

Chakula, vitamini na maji

Kuku wanaohatamia wapewe chakula cha kuku wakubwa wanaotaga (layers mash) cha kutosha muda wote kiwemo kwa kua kuku hawa hutoka wakati tofauti pia majani, mboga-mboga na maji ya kunywa ni muhimu sana. Vyote hivi viwekwe kwenye chumba ambacho kuku wanahatamia ili kumfanya kuku asiende umbali mrefu kutafuta chakula pia kuyaacha mayai kwa muda mrefu.

Hatua za kuhatamisha kuku

 1. Kuandaa viota, uchaguzi wa matetea bora na kuandaa mayai.
 2. Tetea wa kwanza akianza kuhatamia muweke mayai yasio na mbegu ama viza.
 3. Rudia zoezi hili mpaka itakapo fikia idadi ya kuku unao wahitaji.
 4. Baada ya kupata idadi ya kuku wawekee mayai yenye mbegu.

N.B. kuku wote waliochaguliwa kwa ajili ya kuhatamia wawekwe wakati wa usiku kwa sababu ya utulivu uliopo.

Kwa kupitia njia hii kuku mmoja anaweza kuhatamia hadi mayai 20 ukizingatia sifa za kuku huyo. Baada ya kutotoa hatua ya awali ya uleaji wa vifaranga. Kuku wazazi hutengwa na vifaranga ambapo vifaranga hupewa joto na mwanga kwa kutumia taa ya umeme, jiko au kandili. Maji yenye glucose kwa ajili yakuongeza nguvu, pia chakula.

Changamoto

 • Huhitaji sehemu kubwa kwa sababu ili upate vifaranga wengi unahitaji kuku wengi wanao atamia.
 • Kuwepo kwa wadudu kama utiriri na kutopatikana kwa chakula cha kutosha husababisha kuku kutoka toka nje na kusababisha mayai kuharibika.
 • Kuku kupata magonjwa wakati wanapo atamia.
 • Kutokuwa na kipimo cha kupimia mayai yaliyo na mbegu

Ushauri kutoka kwa mfugaji: Wakulima tubadilike na kuanza kufuga kibiashara kwa kua soko la mazao ya kuku wakienyeji lipo. Pia tuweze kuzalisha mayai bora ya kutotolesha, ni muhimu sana yatokane na kuku wako ama kwa mfugaji ambaye una uhakika na ufugaji wake.

Maoni

Naomba niulize utalijuaje yai lenye uwezekano mkubwa wa kutotolewa

naomba niulize utalijuaje yai lenye uwezekano mkubwa wa kutotolewa.

Yai lolote lililotagwa na kuhifadhiwa katika mahala pasafi, bila kushikwa shikwa na mikono yenye mafuta, na kufanya yai lipungue, hutotolewa

naomba mtuwekee mfano (picha) wa kiota bora.

Maada ya kiota bora na picha ipo click sehemu iliyo andikwa zamani utaiona hapo

Nauliza vipi kulishika yai kwa mikono litatotolewa? na kulishika ukiwa umepaka majivu kwenye mikono je?

Kuhusu kushika na majivu hiyo husaidia kutoa unyevu,harufu rangi mkononi isije ika shika kwanye yai kwanini mikono iwea mikavu
-yai liki gusa maji baada ya muda huaribika hivyo ianashauliwa yai la kutotoleshwa lisilowanishwe
Kama likilowa hilo liuzwe kwa ajili ya chakula
-Harufu hufanya kuku kuzila mayai

Naomba niulize majina ya dawa za chanjo ya vifaranga ya gumboro, mahepe(mareks), ndui, kideli

Pia naomba niuliuze chanjo ya kuku wakubwa kama hawakuchanjwa

Kuhusu kinga majina nikama ugonjwa unaokingwa kwa mfano kinga ya kideli
- Kuhusu kuku wakubwa wape kinga ua kideli
Kwa sababu kinga zingine huchanjwa kuku wakiwa wadogo

Vipi kuhusu soko la mayai ya kienyeji dar?

Kuhusu soko usuwaze kwa sababu
Soko la kuku linalingana sehemu zote ni kwa sababu kuku wa kuenyeji wanafugwa wachache

elimu hii ni nzuri sana kwani imenipa mwanga.

Tunashukuru pia unaweza jifunza zaidi na kupata nakala za mkulima mbunifu fingua NAKALA ZOTE pia tunasikika TBC TAIFA saa moja jioni

hivi kuku wanaweza kutaga mapacha wakati wa kutaga

Kuku huweza kutaga yai moja kwa siku. Bali kuna yai laweza kua na viini viwili . Kwa yai hili halifai kuatamiwa na kuku kwani huwa ni kubwa kuku atashindwa kuligeuza.

KIJICHI CHEMCHEM GROUP P.O BOX 46343 DAR ES SALAAM. Ni kikundi cha vijana kilichosajiliwa kisheria na kuendesha shughuli zake za kilimo na ufugaji Mkuranga. Tunaomba mtutumie vipeperushi kwa njia ya posta kupitia hio anuani hapo juu. NAMBA YA MWENYEKITI 0716019555 na 0767945487

Asante bwana Ngosha ila endeleemi kusoma zaidi makala za jarida letu. Tunalifamyia kazi

Mimi ni mfugaji wa kware niko dar kwa yeyote anaeitaji mayai ya kward awasiliane na mimi kwa namba 0656 785345

Ukiwatenga vifaranga na mama yao wale vifaranga wanatakiwa wapate joto utawapatiaje?

Kuku hupata joto kwa
-Kuandaa sehemu maalumu ya kuwaweka vifaramga.
Kwa sababu ili uwe na joto zuri ni vema ukatenga eneo dogo la banda kulingana na vifaranga(broader)

- bulb ya emme

-Jiko la kigai lililo kolea vizuri chenga za mkaa ni mzuri jaziishi haraka
Ila umakini unahitajika hapa kwani vifaranga wan

aweza kufa kwa kuzidi ama kupungua kwa joto

Asante kwa elimu nzuri inayotusaidia ss wafugaji wadogo. Naomba kuuliza hapa kwetu Tz kuna mahali pa kupima ubora wa vyakula vya kuku km mtu anataka kuanza kuchanganya mwenyewe kwa ajili ya kuuza

Cjawai ona watengenezaji kama wanamashine ambayo inapima ubora wa chakula.
Lakini hilo ni wazo zuri kama ukiwa nayo katika biashara yako itawapa uhakika wateja wako.

Tupo pamoja. Ninafuatilia sana makala zenu. Zina msaada mkubwa sana kwetu wafugaji na wakulima. Asante sana.

Tunashukuru sana kwa kutuunga mkono pamoja tulijenge Taifa

Ninaomb mnitumie jarida la mwongozo wa ufugaji wa kuku wa kienyeji email yangu ni [email protected]

naomba kutumiwa kitabu cha mwongozo wa kufuga kuku mimi ni mjasiriamali mdogo ni dar es salaam

Bw. Benson tutakutumia, seleman tunaomba ututumie email yako

Vifaranga wangu wanalemaa miguu na kushindwa kutembea je tatizo hilo linasababishwa na nini?

habari asante Kwa elimu nzuri naomba kuuliza hawa Kuku wasio Na mikia(vibutu) asili yao ni wapi Na utagaji wao ukoje? Mbarikiwe sn

jamani naomba msaada. nimetotolesha vifaranga 50 na kuzingatia joto lishe usafi dawa na chumba au banda. lakini vifaranga wangu wameugua vidonda mdomon na machon tatizo nn naomba mawazo kwa wazoefu

Kupata vidonda kisixho cha kuumia ni muendelezo wa dalili za ugonjwa mwingine kwa maana vidonda haviji kwa siku moja. Kulikua na dalili za awali ya wezekana hukuzi tambua mapema mfano mafua' machozi, uchafu kwenye macho. Hivyo basi matatizo ya macho kuvimba yanatokana na ugonjwa wa macho ama mafua.
Visababishi vyaweza kua ni mabadiliko ya hali yahewa, uchafu nk.

Habarin za leo. Natafuta shamba la kukodi hekar2 maeneo ya mikese morogoro zenye maji kwajili ya umwagiliaji nahitaji kwajili ya kuotesha viungo na mboga mboga(spice&hubs) kwa yeyote mwenye nalo tafadhal awasiliane na mimi kwa 0656-785345 au kwa barua pepe [email protected]. Natanguliza shukrani na Mungu awabariki

Salama?

Kuhusu Mayai, ili yai liweze kutotolewa kuna factor nyingi sana na sio tu utunzaji.

1. Ratio ya Majogoo

2. Aina ya Chakula wanacho kula kuku wakiwemo majogoo

3. Magonjwa mbalimbali

4. Sehemu wanayo tagia-Viota

5. Muda wa ukusanyaji wa mayai Bandani

6. Uhifadhi wa mayai-Yanahifadhiwa vipi?

7. Muda yanayo kaa kabla ya kuingizwa kwenye mashine/Kuku

8. Utaratibu/Hatua za kabla ya kuwekwa kwa mashine

9. Mashine yenyewe/Kuku anaye atamia

na kwa wazalishaji wakubwa kuna Dawa za kutibu mayai kabla hayajawekwa kwenye mashine, ila hizi ni kwa wazalishaji wakubwa.

Chasha Poultry Farm
Kisongo-Arusha-0767-691071

Tunashukuru sana Chasha kwa darasa zuri

Mimi nafuga kware ,nipo oysterbay ,hailesellasie road ,karibu kabisa na kanisa la st.peter.Nauza mayai ya kware shilingi 12,000 kwa tray. Vile tunauza mabata.
Mawasiliano: 0715-496732,0754-496732, 0782-496732.

KARIBUNI

Andika maoni mpya

Plain text

 • Hakuna vishikizo vya HTML vinavyokubaliwa
 • Anuani ya ukurasa kwenye mtandano na anwani za barua pepe hubadilika kuwa viungo moja kwa moja.
 • Mistari na aya zinajipanga zenyewe.